Kwa sasa, haina maana yoyote kukaa na kusimuliana historia ya mambo yaliyotokea nyuma, hasa yale yenye kuleta maumivu ya kijamii, bila kuyatazama kwa mtazamo mpana wenye maono ya mbeleni. Hii ni nadharia nzuri kuitumia katika kuizungumzia historia pana iliyopo nyuma ya pazia la historia ya utumwa.
Historia ya utumwa ni kielelezo dhahiri kwamba bila kujisimamia wenyewe kwa umoja wa nia tunakuwa ni vibaraka wa watu wenye tamaa, ukweli ambao upo wazi hata katika maisha ya kila siku.